Tovuti ya kielimu inayosaidia kukuza Kiswahili miongoni mwa wanafunzi na walimu, kote Afrika Mashariki
LUGHA
Matumizi ya lugha ya Kiswahili yanaangazia sarufi (sheria na kanuni) za lugha hii kwa kuzingatia vipashio vya lugha vinavyotambulika kama vile sauti, aina za maneno, ngeli, nyakati, ukanushaji, uakifishaji, uainishaji wa maneno, aina na muundo wa sentensi na kadhalika.
FASIHI
Fasihi ni moja ya sanaa za lugha. Kwa kuzingatia maana, sifa, na umuhimu wake, katika fasihi tunaangazia vifaa vya Simulizi na Andishi. Miongoni mwa vifaa hivyo, katika ushairi tutazingatia aina za mashairi, muundo wa mashairi na uchambuzi wa mashairi. Hivyo, tutamulika mbinu za lugha na mbinu za sanaa zinazotumika katika fasihi ya Kiswahili.
INSHA
Uandishi wa insha
Ni utuzi wa mfuatano wa tungo zenye mtiririko unaoelezea kuhusu mada fulani. Pengine unaagizwa shuleni ili kumzoesha mwanafunzi kujieleza kwa maandishi. Jifunze jinsi ya kuandika insha mbalimbali - za kubuni na za kiuamilifu.
ISIMU JAMII
Ni tawi la isimumbalo huchunguza uhusiano kati ya lugha na jamii
Comments
Post a Comment